BORN IN THE GHETTO

Masomo Ya Bure

Posted on: November 1, 2008

Tangu serikali ilipochukua jukumu ya kuanzisha elimu ya bure ili iweze kuwanufaisha wanafunzi kimasomo na pia kuondolea wazazi gharama ya kulipa karo, hasa kwa wasiojiweza, wengi wa wananchi walijawa na ghaya bashasha.

Kwangu, kibinafsi, ilikuwa jambo la busara, kwa vile sikufanikiwa kuhitimu masomo yangu wakati ulikuwa unafaa, kwa vile nilizaliwa na kulelewa na wavyele wasiojiweza kifedha. Tulikuwa watoto tisa, na hakuna moja wetu aliyeweza  kukamilisha masomo ya shule ya msingi.

Angalau, idadi ya  watoto ambao huranda randa mjini ingeweza kupunguka ikianzia mimi. Niliamua kujiunga na shule ya msingi iliokuwa katika kitongoji duni, ilhali nilikuwa mwanafunzi wa miaka kadhaa nilionelea heri niweze pata maarifa zaidi shuleni itakayonisaidia siku za usoni.

Wenzangu pia walijiunga na shule ya msingi wakaacha maisha ya kurandaranda mjini. Hapo awali, masomo yalikuwa shwari na tukaweza pata elimu ambayo hatukuwa tumedhania tutawahi bahatika kupata.

Vile muda ulizidi kuyoyoma, ndipo wanafunzi wengi waliendelea kujiunga nasi,na ndipo madarasa yakajaa pomo pomo, ilhali hawakuongezea walimu, idadi yao ilibakia  kama ilivyokuwa hapo awali.

Jambo hili ilianza kuwa hasara kwa wengine wetu, kwa vile kufahamu mambo darasani ilianza kudidimia, kwa kukosa kuhudumiwa kibinafsi. Kwani, watu huwatofauti katika kupata fahamu darasani.

Ni shukrani kubwa sana kwa serikali kwa kugharamia mahitaji ya wanafunzi, ilhali, ndio iweze kuboresha zaidi hili miradi ya masomo ya bure, wanapaswa kuzingatia maswala yanayopendekezwa na walimu pamoja na wanafuzi, ndiposa sisi sote tufaidike maishani kutokana na hii mradi wa elimu bure.

Hongera pia ni kwa shirika ya Undugu Society of Kenya, kwa vile wametukimu na kutufaidisha kimasomo, bila hao, wengi wetu hawangeweza tarajia kuwa na maisha bora siku za usoni. Wameweza tuletea ngao ya maisha, ambapo tunawashukuru sana kwa vyovyote vile.

Translation

Free Education

When the government introduced free education many people were happy because they did not have much money to pay school fees because many people here in Kenya live beyond poverty line. There before you could work in the streets and find many children loitering who are not in school and are supposed to be in school.

The government did some thing good to remember these children who do not have the chance to go to school because of lack of school fees. Since the government has introduced free education when you visit many government schools you will find the classes are loaded.

Many children are happy when they are at school learning with their friends together. What makes me wonder is that when you visit these government schools you will find many children are happy although the way they sit in class is not good since they are loaded.

In these schools students are loaded and this makes them to feel uncomfortable since the class is small and there is no fresh air in that class, especially when it is a sunny day it becomes too hot for them.

When you look at the classes when the students are leaning you find that there is only one teacher and the students are many. This makes the students not to understand the material well but if they are not too many it will easier them to understand what the teacher is teaching.

What I would like to say is that the government to do something so that the number of students can be reduced and they can learn without being loaded. The government should also increase the number of teachers per school since the education is free and many children have gone to school to learn.

Education is good so the government did something positive to introduce free education especially those children who live beyond poverty since they lack the chance to be educated.

Advertisements

1 Response to "Masomo Ya Bure"

I agree with your points about education. The government should realize that the best way for their country to develop they need educated people to run it. By providing their people with an education they are ensuring that the future of the country is a good one. Thus, it is in the best interest of the government to provide funding to increase the amount of schools and teachers.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

My Photos

Advertisements
%d bloggers like this: