BORN IN THE GHETTO

kuzaliwa Na Kuangamia

Posted on: November 15, 2008

Wavyele wanapofanikiwa na kuwapata watoto, wao huwa na furaha mpwito mpwito, kwani, mtoto huchukuliwa kama baraka kubwa katika jamii.

Jambo linalostaajabisha zaidi na kugutusha mno ni kwamba, umaskini umezidi na kupita mizizi, hadi watoto wanaoletwa ulimwenguni wanaangaamia zaidi na kuwa balaa katika jamii.

Umasikini unazidi kila siku uchao nchini Kenya, ilhali nchi yetu inasifika kote ulimwenguni, sio tu kwa minajili ya ustaarabu, bali kwasababu ya watu wakakamavu.Ilhali nchini tumekumbwa na shida za wasiojiweza kifedha.

Wanao fanya kazi za mikono ili angalau waweze kujikimu maishani, wanataabika zaidi kwa vile malipo zao ni duni na haziwezi kuwanufaisha kimaendeleo.Umasikini umewaathiri, mavazi wanazo vaa yameraruka raru raru na viraka viko kote.
Haimanishi kwamba nchini kila mtu hajiwezi kifedha, lakini waliojaliwa  kifedha, hawana budi kuwasaidia wanaohitaji. Ubinafsi umethiri undugu.

Ni jukumu la serikali kuangalia hili swala na kushughulikia kila Mkenya inavyostahili, hasaa wanao taabika. Hili litaweza kuwasaidia watu wengi kuweza kujiepusha na hii ugonjwa wa umasikini.

Ingawa mashambani ndio mlo unapaswa kuwa kwa wingi, Mambo ni mrama huko, kwa vile wakaaji wa mjini ndio wanaangamia zaidi. Hawana fedha kutokana na ukame ulioathiri mimea na kwa sasa hawana cha kuvuna.Ni jukumu la serikali kuweka warsha ili iweze kuwafunza wananchi umuhimu wa kupanda miti, kwa vile huchangia pakubwa katika umuhimu wa mvua.

Serikali kumudu shughuli ya kuwapa watu msaada wa chakula, sio jambo bora zaidi, kwa vile wananchi watakuwa  tu wategemeaji msaada badala ya kutafuta suluhisho wa shida zinazowakumba.Hata hivyo, kama wananchi, tuwe watu wanaojali masilahi ya wengine, kwani, umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.

Translation

Born To Suffer

Poverty is still continuing to destroy many people every day. Kenya is a good country which is united and has peace but many people leave beyond poverty line that makes them not to be able to be stable.

If you look how people leave they show that poverty is still continuing to destroy them, if you look the way they dress their clothes are teared and they do not have some to help them but only themselve.

When you look at those people who are stable you will think that there are no people who live beyond poverty line but if you pass where they live you will see how they are and how they are suffering.

I would like the government to try and help those people who live beyond poverty line so that it can decrease, this will make them not to live in poverty line. If you look in the rural areas many people are suffering from hunger because of lack of  rain, the government should tell people the importance of planting trees so that the trees will attract rain and the hunger will reduce.

Many people are dying because of hunger, the government should help them to get basic needs so that they can survive, you should help your neighbor because all of us we live in peace and love but when we come to help everyone takes his own way.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

My Photos

Advertisements
%d bloggers like this: